Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Ofisi ya Waziri Mkuu yateta na Wadau wa Maendeleo


Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu imekutana na kuwa na kikao cha pamoja na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), Wizara za kisekta na Wadau wa Maendeleo kwa ajili ya kupitia tathmini ya Sera ya maendeleo na huduma kwa Watu wenye Ulemavu, kilichofanyika jijini Dodoma.

Aidha, kikao hicho kililenga kupokea maoni yatakayo wezesha kuboresha taarifa ya tathmini ya maendeleo na huduma kwa Watu wenye Ulemavu.

Akifungua kikao hicho Februari 6, 2024 Jijini Dodoma, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi hiyo Bw. Godfrey Chambo ameshukuru wadau hao kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwasaidia kukuza ustawi wa kundi hilo.