Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Katundu awaongoza Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu kushiriki Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajiara na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu amewaongoza watumishi wa Ofisi hiyo kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika leo Julai 25, 2023 katika uwanja wa mashujaa uliopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameweka jiwe la msingi katika mnara wa mashujaa.

Aidha, Mhe. Rais ameielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu kusimamia ujenzi wa mnara, uwanja wa mashujaana miundombinu ya uwanja huo ili ikamilike kwa wakati na kwa viwango kama ilivyokusudiwa .

Sambamba na hayo, amewahimiza wananchi kuwaenzi mashujaa, kudumisha amani, umoja, mshikamano, utulivu na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.