Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako afungua Mkutano wa 63 wa ATE


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako amefungua mkutano wa 63 wa Bodi mpya ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), leo tarehe 10 Julai, 2023 jijini Dar es salaam.

Akifungua mkutano huo amesisitiza kuwa suala la kufanya kazi la UTATU ni la kisheria ambapo masuala yanayohusiana na kazi na ajira yanajadiliwa na wadau wa UTATU ambao ni; ATE, TUCTA na serikali na kuihakikishia bodi hiyo kuwa serikali itaendelea kuwapa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao.