Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

​Prof. Ndalichako ahimiza ushirikiano wa kuwainua vijana kiuchumi


* Amewataka Vijana wanufaika na Programu ya BBT kufanya Kilimo Biashara kwa kuzingatia tija

Na; Mwandishi Wetu - Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amehimiza ushirikiano baina ya ofisi hiyo na Wizara ya Kilimo ili kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya kilimo.

Prof. Ndalichako akizungumza leo Januari 22, 2024 kwenye hafla ya mapokezi ya vijana 268 wanufaika wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT), katika Shamba la pamoja la Chinangali II Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, amesema na serikali imeanzisha programu hiyo ili kupunguza tatizo la ajira, hivyo wakiwezeshwa kufanya kilimo biashara wataweza kujiajiri, kuajiri wenzao na kuongeza mchango wa sekta ya kilimo katika pato la Taifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema vijana hao wa BBT wamekabidhiwa vifaa wezeshi vya kilimo pamoja na mashamba na wataanza na kilimo cha alizeti katika eneo hilo la Chinangali II.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewahakikishia vijana hao ulinzi na usalama katika shughuli zao.