Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako awataka Vijana wenye Ulemavu kuchangamkia mafunzo ya kukuza ujuzi


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka vijana wenye ulemavu kuchangamkia fursa za mafunzo ya kukuza ujuzi zinazotolewa na Serikali kupitia Ofisi hiyo ili wajikwamue kiuchumi.

Prof. Ndalichako akizungumza Agosti 23, 2023 alipotembelea wanafunzi wa mafunzo ya hayo katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuhakikisha kunakuwepo na elimu jumuishi ili kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu kupata ujuzi utakaowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Aidha, amewataka vijana kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na Halmashauri pamoja na mfuko wa Maendeleo ya Vijana uliopo chini ya Ofisi hiyo ili kupata mitaji itakayowasaidia kujiajiri kupitia ujuzi walioupata kwenye mafunzo hayo.

Amewasihi vijana kulinda amani, umoja, mshikamano na kuwa mstari wa mbele kutangaza kazi nzuri anazozifanya Rais Samia.