Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako: Huduma za Wanachama na Wastaafu kuendelea kuboreshwa


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema serikali imeendelea kuboresha huduma za wanachama na wastaafu nchini ili kutoa huduma bora.

Prof.Ndalichako ameyasema hayo Agosti 12, 2023 kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF) jijini Dodoma.

Amesema kuwa huduma za wanachama na wastaafu zitakuwa zikipatikana kwa njia ya mtandao (TEHAMA) ili kupata huduma kwa wakati na kwa njia rahisi.

Aidha Mhe. Prof. Ndalichako amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira ya dhati ya kuimarisha sekta ya hifadhi ya jamii ili kutoa huduma bora.