Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako: Mazingira mazuri ya Uwekezaji yachagiza ukuaji wa Mfuko wa NSSF


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sekta binafsi yamechochea ukuaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Aidha, Mhe. Ndalichako amesema ukuaji huo umepelekea thamani ya mfuko kuongezeka pamoja na michango ya wanachama.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo Agosti 17, 2023 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya NSSF kwa mwaka 2022/23 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi wa Maendeleo ya Jamii.

Amesema kwa mwaka 2022 mfuko huo uliandikisha wanachama 233,644 hadi kufikia Juni mwaka 2023 kulikuwa na wanachama 243,895 na matarajio ifikapo Juni 2024 ni kuwa na wanachama 277,279.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq, ameutaka mfuko wa NSSF kuhakikisha unaongeza wanachama zaidi hasa waliopo kwenye sekta isiyo rasmi.

Akijibu hoja za wabunge, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amewahakikishia wabunge kuzingatia maoni yao ili kuendelea kuboresha huduma kwa wanachama wake.