Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako: Tutaendelea Kuwahudumia Watanzania kwa Ufanisi


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zake zitaendelea kutekeleza majukumu kwa ufanisi na kuwahudumia wananchi kwa wakati.

Prof.Ndalichako ameyasema hayo Novemba 11, 2023 kwenye kikao cha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Watumishi waliopo chini ya Ofisi yake kilichofanyika katika ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma.

Aidha, Waziri Ndalichako amesema katika kikao hicho kitawasaidia kukumbushana watumishi wajibu wao pamoja na kutengeneza ushirikiano na uhusiano mzuri katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu tutaendelea kuwa timu imara ambayo lengo letu ni kuhakikisha kwamba majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zilizopo chini yake yatatekelezwa kwa ufanisi wa hali ya juu,” amesema