News
PSSSF Yaendelea Kuvutia Mataifa Jirani Kwa Ufanisi Wake wa Uendeshaji
Ujumbe maalum wa Maafisa wa Wizara ya Utumishi wa Umma kutoka Serikali ya Jamhuri ya Uganda umeridhishwa na mfumo wa uendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Hayo yamejili wakati wa ziara ya kikazi ya Maafisa watano toka Serikali ya Uganda waliopo nchini kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu juu ya masuala ya Kinga ya Jamii na uanzishwaji na uendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Ujumbe huo umeongozwa na Robert Ssaka, Mkuu wa Uendelezaji Rasilimali Watu kwenye Wizara ya Utumishi wa Umma Serikali ya Jamhuri ya Uganda walipozungumza na waandishi wa habari Oktoba 07, 2025 jijini Dodoma walipotembelea Mji wa Serikali
Ssaka alisema ziara hiyo ililenga kujifunza namna Tanzania kupitia mfuko wa PSSSF ulivyoweza kufanikisha malengo yake hatua itakayosaidia Uganda kuanzisha mfumo sawa na huo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ya Jamii Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Festo Fute aliwapongeza wajumbe hao kwa kuamua kuja Tanzania kujifunza namna uendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma kwa kuwa umepata mafanikio tangu ulipoanzishwa.
Mwisho.