Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Serikali Yasisitiza Mahusiano na Makundi mbalimbali Kufikia Dira ya 2050


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amesema Serikali imeanzisha Mahusiano kwa lengo la kuunganisha serikali na vyombo vya dini ili kuwaleta watanzania pamoja ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050 kwa Upendo na Amani.

Akizungumza katika Sherehe ya maadhimisho ya miaka 19 ya Kanisa la Neno la Upatanisho ( The Recomciliation Church) Aprili 06, 2026 Jijini Dar es Salaam Waziri Sangu amesema adhma ya serikali katika jukumu jipya la Ofisi hiyo ni kuunganisha serikali na makundi mbalimbali ya kijamii ikijumuisha taasisi za kidini, wadau wa siasa, taasisi zisizo za serikali na mashirika ya kirai.

Katika hafla hiyo, Mhe. Sangu amelishukuru Kanisa hilo kwa mchango wao wa utoaji wa huduma zinazounga mkono Serikali kwa kusaidia Jamii katika sehemu mbalimbali.

“Ampapo ndani ya Miaka 19 ya huduma za Kanisa hili, Serikali imeona kuwa mmefanya kazi kubwa na inathamini michango yenu katika jamii “ amesema Sangu.

Aidha Mahusiano ya Serikali na makundi mbalimbali ya kijamii ni tiba na ni jambo la uponyaji hivyo amewasihi kuwa Milango ya mazungumzo iko wazi muda wote ili kuifikisha Tanzania katika Dira ya 2050.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Alfred Chalamila Ameishukuru serikali kwa kuwaweka karibu na Makundi ya kijamii Kwani ndo imekuwa sababu ya Amani katika Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na dua za kuliombea Taifa katika kila nyakati Zao za ibada.

Naye, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Nicolaus Suguye ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wa viongozi wa dini katika jamii kwa kuwaweka karibu na inawapa matumaini ya kuwa serikali iko pamoja nao.