Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

TANZANIA NA QATAR ZAJADILI AJIRA WAKATI WA KOMBE LA DUNIA


Tanzania imeihakikishia Qatar kuwa ipo tayari kutoa vijana watakaoweza kufanya kazi nchini humo, hususan katika kipindi hiki ambacho mahitaji ya nguvukazi ni makubwa kutokana na nchi hiyo kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Kombe la Dunia yatakayochezwa mwezi Novemba 2022.

Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Katibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu, umebainisha hayo wakati wa kushiriki mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, Dkt. Ahmad Hassan Al-Hamadi kwenye Ofisi za Wizara hiyo Jijini Doha, Qatar tarehe 28 Agosti 2022.

Mazungumzo hayo yamefanyika ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Mkataba wa Kazi uliosainiwa kati ya Tanzania na Qatar mwaka 2014.

Ujumbe huo umeipongeza Qatar kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA litakaloanza mwezi Novemba mwaka huu.

Aidha, Umewafahamishwa kuwa Tanzania imewaandaa vijana wake wenye ujuzi na hivyo kuombwa kupata nafasi za ajira na za viza (visa allocation) kwa ajili ya Watanzania kuweza kuja kufanya kazi Qatar hasa wakati wa kombe la Dunia.

Katika Kikao hicho, viongozi hao pia wamesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili hususan katika maeneo ya uwekezaji na biashara.

Viongozi hao wamefafanua kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya maboresho makubwa ya mazingira ya uwekezaji na biashara, hivyo wametoa wito kwa wafanyabiashara wa Qatar kuja kuwekeza nchini katika maeneo kama vile utalii, kilimo, madini, maliasili, uvuvi na utamaduni.

Wameihakikishia Qatar kuwa Tanzania inazo fursa za biashara na uwekezaji hivyo imekaribishwa Serikali ya Qatar pamoja na wananchi wake kuwekeza Tanzania

Mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, pia umehudhuriwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemed Mgaza na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar, Bi Patricia Kiswaga.

ReplyForward