Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Vijana waaswa kuchangamkia fursa za mikopo


Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana wa Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Dkt. Mwiga Mbesi amewataka vijana kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

Hayo yamebainishwa Agosti 12, 2023 na Mkurugenzi wa Idara hiyo kwenye kilele cha siku ya kimataifa ya vijana Duniani kilichofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe jijini Dodoma.

Amesema serikali inatenga fedha kila mwaka kwa ajili ya vijana kwenye mfuko huo na kupitia mapato ya Halmashauri.