Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Vijana wapongezwa kwa kuchangamkia fursa za BBT


Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu imewapongeza vijana kwa kuchangamkia fursa ya programu ya Taifa ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) inayoratibiwa na Wizara ya Kilimo kwa Kushirikiana na Ofisi hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa Agosti 18, 2023 na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Leonard Mchau alipotembelea Kituo cha mafunzo ya wakulima na kuhimilisha vijana cha Bihawana na Chinangali mkoani Dodoma.

Amesema licha ya baadhi ya vijana hao kuwa na elimu ya juu lakini wameamua kujikita katika kilimo ili kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wao, Wanufaika wa Programu hiyo, Aseiblem Msuya na Baraka Issa , wameishukuru serikali kwa kuwapa mafunzo hayo ya kilimo na kuwahimiza vijana kutumia fursa zinazotolewa na serikali ikiwamo BBT ili kujikwamua kiuchumi.