Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Viongozi Washiriki Hafla ya Tuzo za AOSH 2026, Njombe


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa hafla ya ugawaji Tuzo za Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (AOSH 2026) iliyofanyika Aprili 29, 2026 mkoani Njombe.

Pamoja naye ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Mary Maganga; Naibu Katibu Mkuu, Bi. Zuhura Yunus; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Hawa Mchafu; Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka; na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina.

Tuzo za AOSH hutolewa kila mwaka kutambua na kupongeza maeneo ya kazi yanayozingatia kwa ukamilifu Sheria na Kanuni za Usalama na Afya Kazini.

Aidha, Maadhimiyo hayo yalibeba Kauli Mbiu isemayo”Mazingira Bora ya Kazi Kisaikolojia ni Njia ya Kuimarisha Ustawi wa Wafanyakazi na Kujenga Taasisi Imara”

MWISHO