Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Wafanyakazi wa Hoteli wapewa mafunzo ya huduma ya kwanza


Wafanyakazi 700 wa hotelini mkoani Arusha wamepewa mafunzo ya kutoa Huduma ya Kwanza yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ili kukuza ujuzi wao wa kutoa huduma bora kwa watalii wanaokuja nchini ikiwamo huduma ya kwanza.

Mafunzo hayo yanatolewa kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi iliyopo chini ya ofisi hiyo ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kupaisha sekta ya utalii nchini kwa kuhakikisha watalii wanahudumiwa kwa weledi na ujuzi stahiki.

Akitoa mafunzo ya huduma ya kwanza kwa wafanyakazi hayo, Mwezeshaji Dk.Christopher Nzella, amehimiza wafanyakazi hao kujua namna ya kuwahudumia watu waliopata mshtuko, kuzimia au tatizo lolote la ghafla ya kiafya.

“Ni muhimu kuwa na sanduku la huduma ya kwanza kwenye hoteli zenu kubwa hata nyumbani, mfano mgeni amekuja katoka porini amevimba unampeleka eneo la huduma ya kwanza unampa huduma stahiki, hii itasaidia hata wanaporudi kwenye nchi zao wanasema hatujawahi kutana na huduma bora kwenye hoteli fulani ya Tanzania,”amesema.