Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

WAZIRI MKUU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa ofisi yake alipokutana nao Aprili 10, 2121 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF, Jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa kikao na Viongozi, Wakuu wa Idara na Vitengo na watumishi wa ofisi hiyo.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Prof. Godius Kahyarara (wa kwanza kulia) akiwa poamoja na Manaibu Makatibu Wakuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya (katikati) na Prof. Jamal Katundu wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Waziri Mkuu, Kassim Majiliwa (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jemista Mhagama akieleza jambo wakati wa kikao hicho.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Godffrey Mwambe akieleza jambo wakati wa kikao hicho.

Sehemu ya Watumishi wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakiwasilishwa kwenye kikao hicho kilichofanyika Aprili 10, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la PSSSF, Jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Tixon Nzunda akieleza jambo wakati wa kikao hicho.