Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako aja na utaratibu wa kukutana na Wastaafu Nchini


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, katika kuhakikisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unatoa huduma bora kwa wateja wake, ameielekeza PSSSF hivi karibuni imuandalia utaratibu wa yeye mwenyewe kukutana na Wastaafu na kuongea nao, ili kuzijua kero na malalamiko yao na kuzipatia suluhisho.

“Naanzia hapa Dodoma baadaye nitaenda mikoa mingine, nitaongea na Wastaafu nchi nzima nitakuwa na vituo maalum pamoja na Wataalamu, nitawasikiliza Wastaafu wote watakao kuwa wanajitokeza na lazima watangaziwe ili wajitokeze kwa wingi. Nataka nijiridhishe kero zao ni zipi na zipate ufumbuzi kwa wakati. Lazima katika utendaji wetu tuoneshe kuwaheshimu wastaafu na kuthamini mchango wao kwa Taifa letu”

Ameyasema hayo leo, tarehe 16Mei, 2022, wakati alipokutana na Menejimenti pamoja na Watumishi wa Mfuko huo, jijini Dodoma ikiwa ni ziara ya kufuatilia utendaji wa majukumu ya Taasisi ambazo zipo chini ya Wizara hiyo, ambapo amebainisha kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan tayari maeupa uhai mfuko hivyo wafanyakazi hawanabudi kutoa huduma bora kwa wateja.

“Namshukuru Mhe. Rais ndani ya mwaka mmoja ya uongozi wake amelipa deni lilodumu kwa miaka 20, deni lile la kuchukua wanachama ambao waliingizwa kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakati walikuwa hawachangii na serikali ikaweka mpango wa kulipa michango yao, kiasi cha shilingi trilioni 4.6. Mheshimiwa ameingia madarakani ameweza kutupatia shilingi trilioni 2.17, hii imetupa pumzi na ahueni ya haya tunayofanya”.

Katika hatua nyingine Mhe. Ndalichako ameielekeza PSSSF utaratibu wa kuhakikisha nyaraka za Wastaafu watarajiwa zinakamilishwa mapema ili kuondoa kero kwa wastaafu Amebainisha kuwa pamoja kuwa jukumu lipola Mwanachama na Mwajiri juu ya taarifa zake lakini, Hali hiyo itasaidia kufanya maandalizi ya kuwalipa wastaafu mapema.

Aidha, ameielekeza PSSSF kuwa vifungu vya sheria ya Mfuko huo viangaliwe hususani katika maeneo ambayo vinaeleza kuwa Taarifa ziwasilishwe kabla ya miezi sita ya kustaafu na Mstaafu atalipwa ndani ya miezi 2 baada y akuwasilisha nyaraka zake zilizokamilika. Ambapo hali hiyo inamfanya msataafu kulipwa miezi minne kabla.

Pia, ameiataka PSSSF kuangalia namna bora ya kuwashughulikia Wastaafu ambao vieleezo vinathibitika nyaraka zao za utumishi zimepotea hususani kutokana na majanga kama ya moto, ajali na mafuriko. Aidha, ameitaka PSSF kuendelea na uhakiki wa kidigitali wa Wastaafu ili kujiridhisha kana wanaolipwa kuwa ndio sahihihi.

Mhe. Ndalichako, ameitaka PSSSF kuongeza nguvu ya kufuatilia michango ambayo haijawasilishwa na waajiri, ambapo ameeleza kuwa pamoja na kuwa katika mwaka mpya wa fedha michago hiyo itakuwa ikikatwa moja kwa moja kutoka Hazina, bali amesisitiza orodha ya waajiri ambao hadi sasa hawajawasilisha wafuatiliwe.

Vile vele, Mhe. Ndalichako ameelekeza PSSSF watumie vyombo husika katika kuhakikisha wanakomesha utapeli kwa wastaafu unapfanywa na baadhi ya watu hususani kwa kuwalaghai kuwa wakitoa kiasi cha fedha ili waweze kupata mafao yao bila mapunjo.

Amesisitiza Mfuko huo uendelee na uwekezaji wenye tija hususani kwenye miradi ya Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha karanga ambapo amesisitiza kuongeza ubunifu wa bidhaa zinazo zalishwa kiwandani hapo. Aidha, ameutaka mfuko kutangaza majengo yaliyo waizi ili yaweze kupata wapangaji, kama walivyofanya katika jengo la PSSSF Complex lililopo kwenye barabara ya Sam Nujoma, ambapo idadi ya wapangaji imeongezeka na kuutaka Mfuko kuongeza juhudi ya kusaka wapangaji.

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu ndio msimamizi wa sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini.