Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako ataka Ushirikiano Vyuo vya Ufundi na Waajiri


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako (Mb), amezitaka taasisi zinazotoa mafunzo ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya ufundi Stadi kushirikiana na waajiri ili kukuza na kuimarisha ujuzi kwa wahitimu.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo tarehe 16 Mei, 2023 jijini Arusha katika Ukumbi wa Mount Meru Hotel jijini Arusha wakati akifungua kongamano la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi lililowakutanisha wadau mbalimbali wa Elimu wakiwemo vyuo, waajiri, taasisi za serikali wadau wa maendeleo na sekta binafsi ili kujadili na kubadilishana uzoefu katika kukuza elimu ya ufundi na stadi za kazi kwa maendeleo ya nchi.

Kongamano hili litafanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 16 hadi 17 Mei, 2023 na ni sehemu ya Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayoendelea katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.