Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Waziri Ndalichako atembelea Mabanda ya Washiriki Maonesho ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi wametembelea mabanda ya Washiriki katika maonesho ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika viwanja vya Tumbaku, mkoani Morogoro.

Aidha, viongozi hao walipata fursa kujionea gari la kutolea huduma za afya la OSHA ambalo limerahisisha utoaji wa huduma za afya kwa Wafanyakazi.