Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Waziri Sangu amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Mtaka


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka leo Machi 20, 2026, katika Ofisi za PSSSF, Jijini Dar es Salaam.

Aidha, katika kikao cha viongozi hao wamejadili kuhusu hatua za maandalizi kuelekea sherehe za Mei Mosi, 2026 amabazo zitafanyika kitaifa Mkoani Njombe.

Akizungumza Waziri Sangu amesema, Mei Mosi ni moja ya tukio kubwa na linaweza kuwa ‘brand’ mkoa unaoadhimisha vizuri au vibaya, hivyo ametaka uratibu wa shughuli mbalimbali katika maadhimisho hayo kufuatilia kwa karibu ili wafanye vizuri.

"Nikushukuru kwa kikao hiki nadhani sasa tutakwenda pamoja kila hatua na mimi nitahakikisha kwa upande wangu ninatekeleza wajibu wangu ipasavyo ili kufanikisha jambo hili” alisema Mhe. Sangu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, alisema lengo la kukutana nae ni kumjulisha kuhusu uenyeji wa mkoa wake kwenye sherehe za Mei Mosi kwa mwaka huu wa 2026.

“Baada ya kupokea barua ya Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kuhusu sherehe za Mei Mosi mwaka huu 2026, kama viongozi wa mkoa tukaona ni vema kukutana na wewe Waziri mwenye dhamana ili kukujulisha kuhusu wenyeji wa mkoa wetu kwenye sherehe za mwaka huu,” alisema Mhe. Mtaka

Vilevile, amesema Mei Mosi ya mwaka huu 2026 itakuwa ya Kazi, lakini Kazi inayojenga misingi ya utu kwa watumishi wa umma na binafsi.

Katika kikao hicho alishiriki pia Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Zuhura Yunus, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Stephen Nindi na viongozi wengine wa mkoa huo.