Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Waziri Sangu ataka Mawakala binafsi kufuata mwongozo


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano Deus Sangu amewataka Mawakala binafsi wa Ajira kuzingatia mwongozo wa uratibu wa ajira za nje ya nchi ili watanzania wengi wanufaike na fursa za ajira zinazozalishwa. ‎ ‎Waziri Sangu ameyasema hayo leo Februari 19, 2026 jijini Dar es Salaam wakati alipofanya mkutano na Mawakala binafsi 148 wa ajira za ndani na nje uliolenga kutoa mwelekeo wa Serikali kuhusu uzingatiaji wa uratibu wa kisheria na kimfumo. ‎ ‎ ‎Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inatambua jukumu la Mawakala binafsi kuwa ni nguzo muhimu ya kuwaunganisha watafutaji kazi na waajiri ndani na nje ya nchi pia kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira nchini na kusaidia nchi kujenga uchumi shindani, jumuishi na endelevu. ‎ ‎Akizungumza kwa niaba ya Mawakala binafsi , Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala Binasfi wa Ajira Tanzania (TRAA) Mohammed alisema chama hicho ni mshirika wa serikali katika kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza mapato ya taifa na kuongeza hadhi ya Mtanzania anaefanya kazi nje . ‎ ‎ ‎Kwa upande wake Kamishna wa Kazi Bi. Suzan Mkangwa amesema uwepo wa mwongozo huo ni moja ya hatua za serikali katika kuimarisha huduma za ajira nchini na kwamba ushiriki wa mawakala 148 na kwenye kikao hicho cha Waziri no kutimiza malengo ya Serikali katika kuimairisha mahusiano na kuongeza uwelewa juu ya wajibu wao kisheria na kulinda maslah ya watafuta kazi na maslahi ya taifa kiujumla. ‎ ‎Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Jane Sorogo amesema kufanyika kwa kikao hicho ni mwendelezo wa Idara ya Huduma za Ajira katika kutekeleza dhamira ya pamoja ya Serikali na wadau kuimarisha mifumo ya ajira iliyo salama, halali na yenye kulinda utu na maslahi ya Mtanzania.