Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

ZIARA YA NAIBU WAZIRI UMMY MKOANI SIMIYU AKIPOKEA TAARIFA YA USHUGHULIKIWAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akisisitiza jambo kwa Viongozi wa Mkoa wa Simiyu alipofanya ziara yake ya kikazi mkoani humo kwa lengo la kupokea taarifa ya ushughulikiwaji, ufuatiliaji na uhamasishaji wa masuala ya Kisera, Kisheria na Miongozo kuhusu huduma kwa Watu wenye Ulemavu ikiwemo kuwafikia watu wenye ulemavu Vijijini na Uzuiaji wa Vitendo vya Usafirishwaji na Utumikishwaji wao katika kuombaomba Mitaani.

Sehemu ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi hicho kilichowakutanisha kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu katika Mkoa huo. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu walipokutana kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu katika Mkoa huo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu pamoja na Viongozi wa Vyama vya Watu Wenye Ulemavu katika Mkoa huo wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha kwa ajili ya majadiliano ya pamoja kuhusiana na masuala ya Watu wenye Ulemavu.

Katibu wa Chama cha Watu wenye Ulemavu (CHAWATA) Mkoa wa Simiyu, Ndg. Gerald Makasi (kulia) akichangia jambo wakati wa kikao kazi hicho kilichokuwa kikiongozwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga.