Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Mhe. Sangu ataka Waajiri kusajili Maeneo ya Kazi OSHA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Clement Sangu amewataka waajiri wote nchini kuhakikisha wanasajili maeneo yao ya kazi OSHA ili kutekeleza taratibu za usalama na afya kwa mujibu wa Sheria.

Aidha, ametaka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya waajiri watakaobainika kutosajili maeneo yao.

Waziri Sangu ametoa kauli hiyo leo Disemba 22, 2025 alipotembelea Ofisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), JijiniDar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli zinazotekelezwa na taasisi hiyo.

Vilevile, Waziri Sangu ameigiza OSHA kufanya kampeni maalumu ya usajili nchi nzima ili waajiri wazingatie viwango vya usalama na afya, hivyo kupunguza ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

Kwa upande mwengine, Waziri huyo ametoa rai kwa menejimenti na watumishi wa OSHA kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatoa huduma bora, kufanya kaguzi na kushauri namna bora ya kuandaa na kusimika mifumo itakayowezesha kulinda wafanyakazi dhidi ya ajali magonjwa yanayotokana na kazi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda amempongeza Waziri Sangu pamoja na Naibu Waziri, Rahma Kisuo kwa kuteuliwa kuiongoza Wizara na amemuahudi Waziri kwamba taasisi hiyo ya OSHA itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi katika kulinda afya na usalama mahali pa kazi.

Katika ziara hiyo, Waziri Sangu aliambatana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo pamoja na Kamishna wa Kazi, Suzan Mkangwa.