Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

​Zaidi ya Ajira 9,900 Zazalishwa Mkulazi


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu amekipongeza Kiwanda cha Sukari Mkulazi kwa kuzalisha zaidi ya Ajira 9,900 kwa Watanzania, hatua inayosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajira na kuongeza kipato cha wananchi katika maeneo yanayozunguka kiwanda hicho.

Mhe. Sangu amesema uwekezaji uliofanywa na kiwanda hicho umeleta manufaa chanya kwa Taifa, si tu kwa kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, na kuchochea ukuaji wa uchumi wa ndani kupitia ajira za moja kwa moja 1920 na zisizo za moja kwa moja 8000.

Amebainisha hayo Januari 23, 2026 Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho ambacho kwa sasa uzalishaji umefikia tani 38,000 kati ya lengo la tani 50,000 ifikapo mwaka 2026/2027.

Aidha, Mhe. Sangu amekipongeza kiwanda hicho kwa kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayokizunguka kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii, ikiwemo uanzishaji wa zahanati ambayo siyo tu inawahudumia wafanyakazi wa kiwanda hicho, bali pia wananchi kutoka maeneo mbalimbali, hatua inayochangia kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na kuimarisha ustawi wa jamii kwa ujumla.

Pongezi kwa kuwa na mahusiano mazuri na jamii iliyowazungu kwa kuwapa huduma mbalimbali ikiwemo zahanati ambayo sit u inawahudumia wafanyakazi wa kiwanda hicho, bali na wananchi kutoka maeneo mbali mbali

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Bodi wa Kiwanda hicho Dkt. Hildelitha Msita, ameahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazi, kuongeza uzalishaji na kuimarisha ushirikiano na Serikali ili kuhakikisha sekta ya viwanda inaendelea kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa.

Kwa upande mwingine, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii – NSSF pamoja na Jeshi la Magereza – Jeshi la Magereza, ambao ni wabia wakuu wa kiwanda hicho, wameeleza kuridhishwa na maendeleo yanayoendelea kupatikana kupitia uwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi.

Wamesisitiza kuwa ushirikiano huo umeleta matokeo chanya kwa Taifa kupitia uzalishaji wa ajira, ongezeko la mapato na utoaji wa huduma za kijamii, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine kuhakikisha kiwanda kinaendelea kuwa chachu ya maendeleo endelevu kwa jamii na uchumi wa nchi.