Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Baraza Jipya la Wafanyakazi laagizwa kuzingatia Vipaumbele vya Ofisi


Baraza jipya la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano limeagizwa kuzingatia misingi ya mahusiano mazuri mahali pa kazi, uwajibikaji na uadilifu ili kuongeza ufanisi na ustawi kazini.

Akizindua Baraza hilo leo tarehe 25 Machi, 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amewataka wafanyakazi wa ofisi hiyo ameeleza kuwa vipaumbele vya Ofisi hiyo ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa sheria za kazi nchini, kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008, kuratibu mafunzo ya ukuzaji ujuzi, pamoja na kuratibu fursa za ajira kwa Watanzania nje ya nchi.

Vipaumbele vingine ni kuratibu utekelezaji wa majadiliano ya pande tatu kati ya Serikali, waajiri na wafanyakazi, kufanya mapitio ya sheria mbalimbali za kazi na hifadhi ya jamii, pamoja na kuandaa miongozo ya mahusiano kazini na kuratibu maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).

Sambamba na hayo, Waziri Sangu amezishukuru taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo ambazo ni Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mary Maganga, ameahidi kusimamia utekelezaji wa vipaumbele na majukumu yote ya Baraza ili kuhakikisha kunakuwepo mazingira bora ya kazi na kuongeza tija katika utumishi.

Naye, Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Cde. Rugemalira Rutatina amepongeza Baraza hilo na kuitaka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano kuhakikisha inazalisha wafanyakazi bora, hususan kwa kuzingatia nafasi yake katika kuratibu maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.

Kikao cha kwanza tangu kuanzishwa Wizara hilo kimefanyika tangu kuundwa kwa Baraza hilo kunatokana na mabadiliko ya kimuundo ya Serikali yaliyofanyika Novemba 17, 2025, ambapo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitangaza Baraza la Mawaziri pamoja na Wizara zake, na kuipa Ofisi ya Waziri Mkuu majukumu ya kushughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Mahusiano, hatua iliyolazimu kuundwa upya kwa Baraza la Wafanyakazi.

Pia, katika kikao cha baraza hilo mada mbalimbali zimewasilishwa kwa wajumbe ikiwemo masuala ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).