Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Dkt. Seif asema Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kutoa Huduma Bora kwa wakati


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI (Afya) Dkt. Jafar Rajab Seif amepongeza ubora wa huduma unaoendelea katika banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu Pamoja na taasisi zake katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salam (Sabasaba) 2026.

Amesema hayo leo (Julai 10, 2026) alipotembelea banda hilo na kuridhishwa na huduma ambapo ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda hilo kwa siku zilizobaki ili waweze kujifunza mengi kuhusu majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu .

Akizungumza na waandiahi wa habari mara baada ya kutembelea banda hilo Naibu Waziri huyo alisema banda la Ofisi ya Waziri Mkuu ni banda maalum ambapo mwananchi akifika anapata huduma nyingi na ufafanuzi kwa wakati mmoja jambo ambalo linamsaidia kutatuliwa changamoto zake kwa wakati.

" Wananchi tembeleeni banda la Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo utakuta huduma zote zinazotolewa kwa pamoja na Ofisi ikiwemo TAMISEMI, Sera,Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu pia huduma za Kazi,Ajira na Mahusiano. Fursa hii inapatika kwenye banda jumuishi " alisisitiza Dkt. Seif

Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanaendelea katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa Road Jijini Dar es Salaam yakishirikisha Wizara na taasisi mbalimbali za Serikali na sekta binafsi.