Habari

Ikupa atoa wito kwa Makampuni na Mashirika kusaidia wenye Ulemavu

Ikupa atoa wito kwa Makampuni na Mashirika kusaidia wenye Ulemavu

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa (Mb), ametoa wito kwa wadau sekta binafsi, Makampuni na Mashirika mbalimbali kuwasaidia watu wenye Ulemavu, ili kuwawezesha kukidhi mahitaji yao ikiwemo kuendeleza shughuli na vipaji vyao.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Ikupa alipokuwa akikabidhi Bajaji kwa Mama Leonea Leonard ambaye ni mlemavu wa miguu, ambapo amesema Bajaji hiyo ameipata kwakushirikiana na mdau baada ya kumweleza kuhusu shida ya Mama huyo.

“Wahitaji wako wengi nchini, unaweza kumsaidia Mama leonia au unaweza kumsaidia mhitaji mwingine leo tumempatia Bajaji inaweza kumsaidia katika shughulizake lakini pia bado analo hitaji lakusaidiwa kurecord nyimbo zake, tunaomba mdau mwingine aweze kujitokeza amsaidie aweze kurecord,‘’Alisema Ikupa

Kwaupande wake Mama Leonea Leonard, amemshukuru Mhe. Stella Ikupa, kwa moyo wake wa kujali watu bila kujali kuwa ni ndugu yake ama kuwa anaulemavu bali anasaidia watu wote, amesema watu wengi wanauwezo kifedha hivyo aliomba waweze kujitokeza kusaidia wenye Ulemavu.