Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Kamati ya Bunge Yapongeza WCF Usajili Waajiri


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) uliopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wa kusajili waajiri kwa asilimia 92.2.

Akizungumza leo Machi 23, 2023 katika kikao cha kamati cha kupokea utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo na taasisi zake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq, ameupongeza mfuko kwa hatua hiyo na kuahidi kuendelea kuishauri vyema serikali.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameahidi Ofisi yake itaendelea kushirikiana na kamati hiyo ili ifanye kazi yake ya kuishauri serikali.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya WCF, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Dk.John Mduma, amesema hadi sasa asilimia 92.2 ya waajiri wamesajiliwa.

Amesema usajili wa waajiri umeongezeka kutoka waajiri 5,178 sawa na asilimia 17.2 kwa mwaka 2015/16 hadi kufikia waajiri 27,786 sawa na asilimia 92.2 kwa mwaka 2021/22.

Aidha, amesema katika kipindi cha miaka saba ya utekelezaji wa mfuko huo umelipa fidia kiasi cha Sh.Bilioni 44 huku kiwango cha fidia kwa mwaka kimeongeza kutoka Sh.bilioni 1.5 hadi Sh.Bilioni 13.

“Mapato ya uwekezaji yameongezeka kutoa Sh.bilioni 1.6 tulivyoanza hadi kufikia mwaka 2021/22 ilifikia Sh.bilioni 74,” amesema