Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

KAMPUNI YA GRUMETI RESERVE YATAKIWA KUTOA MIKATABA KWA WAFANYAKAZI AMBAO HAWANA MIKATABA


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Kitalii ya Grumeti Reserve kutoa mikataba kwa wafanyakazi wake wasiokuwa na mikataba ya Ajira ndani ya masaa 48 .

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akishughulikia akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya Grumeti Reserve alipofanya zira ya kukagua utekelezaji wa sheria za kazi.

Naibu Waziri Mavunde amefikia ametoa maagizo hayo Wilayani Serengeti, Mkoani Mara wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria za kazi katika Kampuni ya Grumeti Reserve ambapo baada ya kusikiliza maoni ya wafanyakazi na kubaini baadhi hawana mikataba ya Ajira,Menejimenti ya Kampuni hiyo imeahidi kuwapatia wafanyakazi hao mikataba ndani ya masaa 24 muda ulioongezwa mpaka masaa 48 na Naibu Waziri Mavunde ili kuwapa muda wa kutayarisha mikataba hiyo kwa usahihi.

Pamoja na Agizo hilo Naibu Waziri Mavunde ameiamuru Kampuni hiyo kulipa faini ya Tsh 1,400,000 kwa kosa la kuwafanyisha kazi wafanyakazi 28 bila kuwa na vifaa kinga kinyume na matakwa ya Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi.

Aidha katika nyakati tofauti wafanyakazi hao wameishukuru Serikali kwa kusikiliza changamoto zao na kuomba utekelezaji wa maagizo hayo usimamiwe ili kupata haki zao za kimsingi.