Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Katibu Mkuu Utumishi atembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi ametembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano leo tarehe 22 Juni, 2026 ili kuona huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma.

Akiwa katika Banda hilo, Katibu Mkuu Mkomi ameeleza kufurahishwa na Elimu pamoja Huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 pia amewashauri watumishi wa Ofisi hiyo kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi wanaotembelea Maadhimisho hayo.

Kwa upande wake, Afisa Rasilimali Watu Bi. Suzan Kimambo alimuhakikishia kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano itaendelea kutoa huduma bora sambamba na kuelimisha wananchi kuhusiana na Sera, Sheria, Miongozo na Programu zinazotekelezwa na Ofisi Hiyo.

Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yatafikia tamati kesho Juni 23,2026. Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni: “ Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu”