Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Kenya atembelea Mfuko wa PSSSF, NSSF na WCF


Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko na ujumbe wake wametembela Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Ziara hiyo inalenga kubadilishana uzoefu katika masuala ya sekta ya hifadhi ya jamii sambamba na kuangalia maeneo ya ushirikiano katika masuala yanayohusu sekta hiyo.

Katibu Mkuu Kaituko amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Emmanuel Humba jijini Dar es Salaam, ambapo mazungumzo yao yalijikita katika kubadilishana uzoefu kuhusu sekta ya hifadi ya jamii.

Mbali na hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko alitumia fursa hiyo kupongeza kuhusu juhudi zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hatua kubwa ya kuimarisha sekta ya hifadhi ya jamii.

Naye Mkurugenzi wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba amesema uwepo wa vikao hivyo vya majadiliano kutasaidia kujenga uwezo katika kuimarisha na kukuza sekta hiyo sambamba na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Kenya.