Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Maganga aongoza mazishi ya Wakili Swai


‎Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Bi. Mary Maganga

‎ametoa pole kwa familia pamoja na watumishi wa Ofisi hiyo katika Ibada ya mazishi ya Marehemu Wakili Charles Boaz Swai iliyofanyika katika kanisa la Pentecostal Holiness Mission Shilo - Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo Ijumaa, Mei 30, 2026.

‎Aidha amewasihi watumishi kuiga mfano wa marehemu Swai katika utendaji kazi na kufanya majukumu kuwa ni wito.

‎Katika hatua nyingine Bi.Maganga amewapongeza wazazi wa marehemu Charles kwa kumlea kijana katika maadili mazuri ya uchapakazi, lakini pia amemuomba mjane wa marehemu Bi.Herieth Juma Hoza kuendelea kuwalea watoto katika maadili mazuri ili waige mazuri ya marehemu baba yao.

‎Naye aliyekuwa Mwanafunzi mwenzake wa Shule ya Sheria kwa vitendo Deogratius Kapufi akitoa salamu zake alisema Marehemu Swai alitumia taaluma yake kusaidia jamii ya kitanzania kupata haki zao mujibu wa sheria.

‎Marehemu Wakili Charles Swai alizaliwa mwaka 1989 ambapo katika utumishi wake alifanikiwa kuanzisha kampuni binafsi ya uwakili ya Competency International. Hadi umauti unamkuta alikuwa Afisa Sheria katika Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano ambapo ameacha mke na watoto watatu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.