Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

MAJADILIANO KUHUSU MCHAKATO WA KURIDHIA MKATABA WA KIMATAIFA WA MARRAKESH


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amkutana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wasioona Tanzania na kujadili kuhusu mchakato wa kuridhia mkataba wa kimataifa wa Marrakesh.

Mkataba wa Marrakesh ulipitishwa rasmi katika ngazi ya Umoja wa Kimataifa Mnamo tarehe 27 Juni, 2013 katika mkutano uliofanyika huko Marrakesh nchini Morocco.

Lengo la mkataba wa Marrakesh ni kusaidia na kuwawezesha Watu wenye Ulemavu wa kusoma maandishi katika mfumo ulio rafiki kwao.

Aidha, umeweka masharti kwa nchi wanachama kuwawezesha walemavu kupata habari kwa urahisi, kusoma vitabu na machapisho ya kawaida katika mfumo rafiki kwao.

Mkataba huu utawawezesha idadi kubwa ya Watanzania wasioona na wenye ulemavu wa kusoma (persons with print disabilities) kupata habari na elimu kwa kusoma vitabu na machapisho katika mfumo rafiki kwao.

Kutoa ufahamu kwa umma kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo watu wenye ulemavu wa kusoma maandishi na hivyo jamii itahamasika kujitolea kwa hali na mali kusaidia utatuzi wa changamoto hizo.

Kuwezesha watu wenye ulemavu wa kusoma kufikiwa na kupata habari kwa urahisi na katika mfumo rafiki kwao hususan katika masuala muhimu ya jamii na taifa kwa ujumla.

Upatikanaji wa teknolojia ya kisasa na ujuzi kutoka nchi wanachama na hata nakala za vitabu zilizowekwa kwenye mfumo rafiki kwa walengwa zitaweza kuletwa nchini. Hii itaongeza upatikanaji wa vitabu na machapisho katika mfumo rafiki kwa walengwa wote duniani.