Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

MATUKIO KATIKA PICHA UZINDUZI WA MBIO MAALUM ZA MWENGE WA UHURU 2021 KATIKA UWANJA WA MWEHE MKOANI KUSINI UNGUJA


Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akizindua Mwenge wa Mbio Maalum za Uhuru 2021 katika Uwanja wa Mwehe kwa lengo la kuzindua Mbio za Mwenye wa Uhuru 2021 Mkoani Kusini Unguja Zanzibar Mei 17, 2021.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na kushoto kwake ni Kaimu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Leila Mussa.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2021 Luteni Josephine Mwambashi wakati wa uzinduzi wa Mbio hizo za Mwenge huo.

Wakimbiza Mwenge 2021 wakiingia uwanjani wakati wa uzinduzi huo.


Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akihutubia wananchi wakati wa Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 Mkoani Kusini Unguja Zanzibar Mei 17, 2021.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 Mkoani Kusini Unguja Zanzibar Mei 17, 2021.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Leila Mussa akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya uzinduzi huo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga wakifuatilia matukio mbalimbali katika Uwanja wa Mwehe Mkoani Kusini Unguja.

Matukio mbalimbali ya burudani yakiendelea katika Uzinduzi wa mbio maalum za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika katika Uwanja wa Mwehe Mkoani Kusini Unguja.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Mwehe kwa lengo la kuzindua Mbio za Mwenye wa Uhuru 2021 Mkoani Kusini Unguja Zanzibar Mei 17, 2021.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdallah akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili katika uzinduzi wa mbio za Mwenge Mkoani Kusini Unguja Mei 17, 2021.

Vijana wa Skauti wakimvika Skafu ya Heshima mgeni Rasmi wa Uzinduzi wa Mbio za Mwenge Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdallah mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Mwehe kwa ajili ya Uzinduzi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru 2021 katika mkoa wa Kusini Unguja Mei 17, 2021.