Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Katambi aongoza kikao kazi cha tathmini na mikakati ya Utekelezaji majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya ofisi hiyo hii leo tarehe 23 Disemba, 2022 katika jengo la OSHA, jijini Dodoma.

Lengo la kikao kazi hicho ni kufanya tathmini na kupanga mikakati ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo.

Akizungumza na menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Katambi amewataka viongozi hao kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, ufanisi, kushirikiana na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao ili kufikia matarajio ya Serikali na wananchi wanaowahudumia.