Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Mhe. Ndejembi: Tutahakikisha Mikopo ya Asilimia 10 inawafikia Vijana na Watu wenye Ulemavu


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Ofisi hiyo itashirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika kuwezesha vijana na wenye Ulemavu Mikopo inayotolewa na Halmashauri ili wafanye shughuli zenye tija.

Mhe. Ndejembi amesema hayo wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2024/25, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 15, 2024.

Aidha, Waziri Ndejembi amesema kuna nafasi kubwa ya kuwakuza vijana wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi kutokana na fursa mbalimbali kupitia fedha zinazotolewa na Serikali anayoiongoza Rais Samia.

Amelihakikishia Bunge kuwa, Ofisi yake itaendelea kuratibu Wizara za Kisekta ili vijana wengi nchini waweze kunufaika na fursa zinazotolewa na serikali yao katika miradi ya kimkakati, kilimo, madini, mifugo na uvuvi.

Kwa upande mwengine, Mhe. Ndejembi alisema Ofisi hiyo kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira nchini (TaESA) wanaendelea na majadiliano na nchi mbalimbali ili kuona namna ya kupata fursa za watanzania wengi kuajiriwa nje ya nchi.