News
wanawake OWM-KAM waunga mkono maendeleo ya taifa dira 2050
Wanawake kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano (OWM–KAM) wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 08, 2026 kwa kusisitiza umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika kuunga mkono maendeleo ya taifa kupitia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2050 ya Tanzania
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo yaliyobebwa na Kauli mbiu Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kugika Dira 2050 ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.
Maadhimisho haya yanalenga kujenga uelewa wa kuwekeza katika maendeleo jumuishi kwa kutambua na kutekeleza haki za wanawake na wasichana kwa vitendo.
Maria Nkangali, Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Kazini, amesema kuwa kupitia kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka 2026 amejifunza mambo mengi muhimu, na ametoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika kuendeleza masuala ya kijamii na maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake, Lucy Murro, Msaidizi wa Kumbukumbu, kutoka Ofisi ya Waziri Kazi, Ajira na Mahusiano amemshukuru Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, kwa kuendelea kuwainua wanawake kwa kuwapa fursa na nafasi katika sekta mbalimbali za uongozi na maendeleo nchini
Aidha, Evodia Sanga, Afisa Hesabu Mwandamizi, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano amewahimiza wanawake wote wanaopewa nyadhifa mbalimbali za uongozi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kujituma ili kuendelea kulijenga taifa na kuchangia kukuza uchumi wa nchi.
