Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

NAIBU WAZIRI KATAMBI AWAHAMASISHA WADAU KUICHANGIA TIMU YA TEMBO WORRIORS


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amewahamisisha wadau kujitokeza na kuchangia timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Watu wenye Ulemavu - Tembo Warriors ili ifanikiwe kushinda mashindano Kombe la Dunia nchini Uturuki ambayo itashiriki michuano hiyo mwaka huu itakayoanza Septemba 30 hadi Oktoba, 09 nchini humo.

Mhe. Katambi akiongea na Timu hiyo kwa lengo la kuwahamasisha na kuwaaga kuelekea nchini Uturuki kwa maandalizi ya michuano hiyo, amefafanua kuwa Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ipo pamoja na Watu wenye Ulemavu na imetoa zaidi ya Mil. 150, ili kuhakikisha wanapata ushindi katika michuano hiyo.

“Tunaomba wadau hususani Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali, Sekta Binafsi tuwasaidie hawa Tembo warriors ili wawe washindani kwenye michuano hiyo”.

Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kuwahamasisha wadau kuisaidia timu hiyo ili iweze kuimarika kimataifa na kuiweka nchi ya Tanzania katika Ramani ya michezo kimataifa