Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AITAKA JAMII KUTOWAFICHA WATU WENYE ULEMAVU WAKATI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga,ameitaka jamii kuacha kuwaficha watu wenye ulemavu wakati wa Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwakani.

Kauli hiyo ameitolea leo June 24, 2021 wakati akifungua semina ya iliyolenga kujadili mustakabali wa ujumuishaji wa Watu wenye Ulemavu kuelekea Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Naibu Waziri Ummy amesema kuwa kutokuwa na takwimu sahihi za Watu wenye Ulemavu kumepelekea kuwa na changamoto ya utoaji huduma kwa kundi hilo kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi za kutambua walipo, aina ya ulemavu walionao na mahitaji yao, hivyo ili kuwezesha kupata takwimu sahihi za kundi la watu wenye ulemavu zitakazotumika kutekelezea mahitaji yao kwa ufanisi lazima jamii iache tabia ya kuwaficha.

”Kumekuwepo na vitendo kwa baadhi ya wanajamii kuwaficha watu wenye ulemavu wakati wa kipindi cha Sensa ya watu na makazi, kitendo hicho wanaikosesha serikali kupata takwimu sahihi ambazo zingetumika kuwasaidia katika kero mbalimbali zinazaowakabili” amesema Mhe.Ummy

Ameongeza kuwa agenda moja wapo katika Malengo ya Maendeleo endelevu 2030 ni kuhusu suala la asiachwe mtu nyuma “Leave no One Behind”. Agenda hii inatilia mkazo suala la kuwa kuwapa kipaumbele wenzetu wenye ulemavu katika shughuli mbalimbali.

“Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika 2022 itachangia kwa kiasi kikubwa kuwa na takwimu sahihi za watu wenye ulemavu nchini kama watu wenye ulemavu watashirikishwa kikamilifu bila mtu yoyote nyuma,” ameeleza

Amefafaanua kuwa, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu umeelekeza pia uwepo wa takwimu sahihi za Watu wenye Ulemavu kunachangia kujipanga vizuri katika kutoa huduma bora kwa kundi hilo.

Pia ameeleza kuwa Serikali imeendela kuwapa kipaumbele Watu wenye Ulemavu katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ustawi wa Watu wenye ulemavu katika katika kuwaleta maendeleo yenye uwiano katika jamii.

“Kwenye Ilani ya Chama Tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye ibara ya 94 na 95 imeelezea namna serikali inavyowatambua watu wenye ulemavu na imeendelea kusisitiza na kutilia mkazo usawa na haki zao,” alieleza

Sambamba na hayo ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika bajeti yam waka wa fedha 2021/2022 imetenga fedha ya kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la sensa ya wat una makazi nae neo moja wapo litakalosimamiwa ni uwepo wa takwimu za watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa serikali Dk. Albina Chuwa amesema kuwa katika Sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwakani, wamejipanga kuhakikisha kila kundi linajumuishwa ili kuwa na takwimu sahihi kwa ajili ya kulisaidia Taifa kutekeleza majukumu yake.