Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

NSSF YATAKIWA KUTOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII KWA WATANZANIA WOTE


Serikali imelitaka Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii NSSF kutoa elimu zaidi kwa wananchi kuhusiana na faida za kujiunga katika hifadhi za jamii nchini.

Hayo yameswemwa na Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Sera,Bunge,Ajira ,Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Jenister Mhagama kwenye wiki ya Taifa ya maonesho ya wiki ya vijana yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga ambapo amesema kuwa bado watanzania wengi hawana elimu ya kutosha kuhusiana na kujiwekea akiba ya uzeeni na faida zake hivyo NSSF inaoaswa kuhakikisha inatoe elimu hii.

“Nawataka NSSF muhakikishe elimu hii mnaitoa ipasavyo na iwafikie watanzania wote nchini ,mwende vijijini huko muelekeze wananchi nao wapate uelewa wa hifadhi za jamii na faida zake”alisema Waziri Muhagama.

Mhagama amesema kuwa NSSF ndio inajukumu sasa la kuandikisha wananchi walio kwenye sekta isiyo rasmi hivyo wahakikishe wanawafikia wananchi wengi waliopo kwenye sekta hiyo na hasa wa vijijini na kuwapatia uelewa na waweze kujiunga na kufaika na mafao yote ya NSSF.

Kwa upande wake kaimu meneja wa NSSF mkoa wa TANGA ,Aisha Nyemba mpaka sasa wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kujiandikisha katika mpango wa hiari ambao utawawezesha kufaidika na mafao mbali mbali ikiwemo mafao ya matibabu.

Kwa mujibu wa Nyemba mpaka sasa NSSF imeandikisha vikundi vya wajasiriamali idadi ya 47 katika mpango wa hiari na wanachangia michango yao kila mwezi ambapo pia juhudi zinaendelea kuhakikisha wanafikia vikundi vingi vya wajasiriamali katika mkoa wa Tanga.

Maonyesho haya ya Taifa ya wiki ya vijana yamefikia kilele chake oktoba 14 mwaka huu ambapo yataendana na sherehe za uzimaji wa mwenge kitaifa katika uwanja wa Mkwakwani na kuenzi miaka 19 ya kifo cha Rais wa kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.