Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

PICHA ZA MATUKIO: KIKAO CHA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja mbalimbali za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokutana kupokea na kujadili masuala yanayohusu muundo na majukumu ya ofisi yake, kikao kimefanyika tarehe 22 Januari, 2021 Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo, kilicholenga kupokea na kujadili muundo na majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kilichofanyika katika ukumbi Namba 9 wa kumbi za Bunge Jijini Dodoma.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe.Elibariki Kingu akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Khadija Shaban akichangia hoja kuhusu changamoto ya upatikanaji wa mafuta maalum kwa ajili ya watu wenye ualbino wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Manaibu wake na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ndg. Andrew Massawe wakifuatilia hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa kikao hicho.