Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako Afanya Ziara Ofisi za ATE Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kuzungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) akiwa ameambatana na Naibu Waziri katika Wizara hiyo Mhe. Patrobas Katambi (Mb) Januari 25, 2022.

Mhe. Waziri amefanya mazungumzo na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya ATE ikiongozwa na Mwenyekiti Bi. Jayne Nyimbo pamoja na Menejimenti ya ATE ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu Bi. Suzanne Ndomba- Doran.

Katika hotuba yake Mhe. Waziri ameipongeza ATE kama mdau wa UTATU kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwa Wizara hiyo katika kuboresha Sekta ya ajira na kazi nchini na kuwasisitiza waajiri wote nchini ambao bado hawajajiunga na ATE kufanya hivyo ili kufaidika na huduma za ATE.

Katika salamu zake Bi. Suzanne Ndomba amemshukuru Mh. Waziri na ujumbe wake kwa kutembelea Chama cha Waajiri katika siku zake za awali katika Wizara hiyo lakini pia alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuigawanya Wizara na kuitenganisha na Sera, Bunge na Uratibu kwani italeta wepesi wa kiutendaji katika masuala ya kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.