Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

Prof. Ndalichako Afungua Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Fursa Mkoani Mtwara


Waziri wa nchi Ofisi wa Waziri Mkuu-Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amefungua maonesho ya Biashara Uwekezaji na Fursa , katika viwanja vya Mashujaa Park mkoani Mtwara ambapo amewataka wajasiriamali mkoani humo kuchangamkia fursa za biashara zilizopo mkoani humo.

Aidha amewata wajasiriamali hao kuwa wabunifu na kutumia teknolojia itakayo wasaidia kuzalisha zaidi na kwa gharama nafuu ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na la nchi za jirani zinazoizunguka nchi yetu.