Habari

SERIKALI KURASIMISHA UJUZI KWA MAFUNDI NCHINI KUTUMIA PROGRAMU YA MFUMO WA UTAMBUZI NA URASIMISHAJI UJUZI (RPL)

SERIKALI KURASIMISHA UJUZI KWA MAFUNDI NCHINI KUTUMIA PROGRAMU YA MFUMO WA UTAMBUZI NA URASIMISHAJI UJUZI (RPL)

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) katika utekelezaji wa programu ya RPL imedhamiria katika awamu ya kwanza kuwafikia na kurasimisha ujuzi kwa takrabani watanzania 10,000 kwa Mwaka 2019/2020.

Hayo yamesemwa leo katika ukumbi wa Royal Tughimbe Jijini Mbeya na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakati akifungua kongamano la mafundi wa Mkoani Mbeya, ambapo alibainisha kwamba Serikali inatekeleza programu ya kurasimisha Ujuzi kwa watu wenye Ujuzi lakini ambao hawajapitia katika mfumo rasmi wa mafunzo ya ufundi kwa kuwapatia vyeti vya ufundi pasipo wao kusoma chuo cha ufundi hasa baada ya kuwa wamepitishwa na wakufunzi na wataalamu kutoka VETA.

"Lengo letu kama Serikali ni kuwajengea uwezo na ujuzi watanzania wengi zaidi ili washiriki kama nguvu katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile ujenzi wa Reli (SGR), mradi wa kufua umeme wa Stiegler's Gorge na miradi mingine mikubwa nchini, alisema Mavunde

Akiwasilisha taarifa fupi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Fundi Smart Bw. Fredy Herbert Pole alieleza lengo la kukusanya mafundi wao ni kuwajengea uelewa kwa kuwapa elimu ua masuala ya fedha, afya na sheria. Vilevile kuwatengenezea mfumo mzuri wa kufanya kazi zao za kila siku kwa kuzingatia weledi, taratibu na sheria.