Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

​Serikali yawaaga vijana 228 wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi


Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Zuhura Yunus amewaaga vijana 228 wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi na amewataka kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania.

Aidha, vijana hao wamepata fursa ya ajira katika nchi ya Oman, Qatar, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Denmark na Ujerumani.

Amesema, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya ajira kwa Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi, na kufanikiwa kuwaunganisha zaidi ya vijana 1,638 na fursa za ajira ndani ya miezi mitatu.

Amewasihi vijana kuchangamkia fursa halali, kufuata taratibu za kisheria, kujiandikisha NSSF, kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia muda.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TaESA, Bi. Jane Sorogo, amesema vijana hao wamepatiwa mafunzo ya maandalizi ili kuwa wafanyakazi wachapakazi na kuenzi utamaduni wa Tanzania.

Naye, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bw. Omary Mziya, amewahimiza kuendelea kuchangia NSSF wakiwa ughaibuni kupitia mifumo ya Tehama.

Awali, Mwenyekiti wa Mawakala wa Ajira nchini, Bw. Abdallah Mohamed, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri na kuwasihi vijana kufuata taratibu zilizowekwa ili kulinda masilahi yao.