Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Tanzania yaongoza Ushirikiano wa Kijamii EAC


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa mwenyeji wa ushirikiano wa kijamii ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kwa kufanyika kwa Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta linaloshughulikia Masuala ya Kijamii ulioanza tarehe 2 hadi 7 Julai 2026 jijini Dar es Salaam

Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri, Makatibu Wakuu na wataalamu kutoka nchi wanachama wa EAC, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kikao cha Baraza la Mawaziri wa Kisekta, Mhe. Rebecca Alitwala Kadaga, ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu wa kwanza na Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Uganda.

Aidha, Tanzania iliwakilishwa na Mhe. Dkt. Eveline Munisi, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano pamoja na Mhe. Joel Nanauka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, ambaye aliongoza ujumbe wa kitaifa.

Katika kikao hicho, viongozi kutoka Wizara za Kisekta walijadili na kupitisha nyaraka muhimu za kisera, ikiwemo

Sera ya Kinga ya Jamii ya EAC 2026, Sera ya Vijana ya EAC 2026, Hadidu za Rejea za Baraza la Kisekta na Mpango Mkakati wa Kisekta wa Jinsia na Maendeleo ya Jamii. Ambapo pia kulikuwa na mapendekezo ya kuanzishwa kwa Mabaraza ya Kikanda ya Vijana, Watoto, Watu Wenye Ulemavu na Wanawake

Hatua hizi ni msingi wa kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta ya kijamii kuhakikisha kwamba Sera na Mipango ya pamoja inatekelezwa kwa manufaa ya wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mkutano huu ni mwanzo wa safari mpya ya kuunganisha nguvu za kijamii na kiuchumi kwa nchi wanachama, Kwa kuwa utekelezaji wa Sera hizi utaleta mabadiliko chanya kwa vijana, wanawake, watoto na makundi maalum katika ukanda huu.