Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Tanzania yashiriki Kikao cha Kamati ya utekelezaji wa viwango vya Kazi, Geneva


Tanzania imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kusimamia haki na staha katika sekta ya kazi kwa kushiriki kikao cha Kamati ya Utekelezaji wa Viwango vya Kazi. Kikao hicho ni sehemu ya Mkutano Mkuu wa 114 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaoendelea jijini Geneva, Uswisi.

Wajumbe katika kikao cha leo Juni 2, 2026 wamejadili masuala muhimu yakiwemo:

-Mjadala wa jumla kuhusu ripoti kuu ya Kamati ya Mkutano, Maadhimisho ya miaka 100 ya ajenda ya Kazi zenye Staha,Tathmini ya jumla ya utekelezaji wa viwango vya kazi kimataifa na Wajibu wa nchi wanachama katika kuwasilisha taarifa na kutekeleza majukumu ya viwango vya kazi.

Katika kikao hicho Tanzania imewakilishwa na wataalam na viongozi waandamizi kutoka sekta ya kazi na mahakama wakiongozwa na Mhe. Dkt. Yose Joseph Mlyambina Jaji wa Mahakama ya Rufani , Bi.Suzan Mkangwa Kamishna wa Kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano ,Bi.Khadija Mwenda Mtendaji Mkuu, Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA)

ma Bw. Usekelege Mpulla Mkurugenzi, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA)

Tanzania ni mwanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) na pia ni mjumbe wa Bodi ya Magavana inayowakilisha nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Mkutano Mkuu wa 114 unawakutanisha wawakilishi wa Serikali, Waajiri na Wafanyakazi kutoka nchi wanachama 187 kwa lengo la kuweka mikakati ya kuboresha mazingira ya kazi duniani.

Ushiriki huu unaimarisha nafasi ya Tanzania katika kuchangia uundaji na utekelezaji wa sera za kazi zenye staha kimataifa.

Mwisho.