Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Ushirikiano wa Afrika na Nchi za Ghuba wafungua fursa za Ajira


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu, amesema ushirikiano kati ya Afrika na nchi za Ghuba (GCC+) umekuwa muhimu katika kukuza fursa za ajira na maendeleo ya kiuchumi.

Mhe. Sangu amesema hayo wakati akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni iliyowakutanisha viongozi na wadau mbalimbali wanaoshiriki Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue, unaolenga kubadilishana uzoefu na kuendeleza ushirikiano katika masuala ya uhamaji wa nguvu kazi wenye haki na endelevu kati ya Afrika na nchi za GCC+.

Aidha, Waziri Sangu amesema ushirikiano unaojengwa kupitia mkutano huo unapaswa kuendelea zaidi ili kuleta matokeo chanya kwa wananchi wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi.

“Uwepo wa viongozi, wawakilishi na wadau mbalimbali katika hafla hii unaonesha dhamira ya pamoja ya kuimarisha mahusiano na kutafuta maeneo mapya ya ushirikiano katika masuala ya kazi na ajira,” amesema.

Kadhalika, amesisitiza umuhimu wa kutambua maeneo muhimu yanayoweza kuendelezwa kwa pamoja, ikiwa ni pamoja na kukuza fursa za ajira na kubadilishana ujuzi na uzoefu.