Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Employment and Relations

News

Vijana wakabidhiwa vitendea kazi kukuza ujuzi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amekabidhi baadhi ya vitendea kazi kwa vijana 84 walionufaika na ajira nje ya nchi chini ya Programu ya COMHESWA hafla iliyofanyika katika Hotel ya Peackok Hotel Dar es Salaam Januari 09,2026.

Wanufaika wa programu maalum ni vijana ambao walihudhuria Mafunzo ya Amali na ujasiriamali yanayotolewa na COMHESWA kwa lengo la kuwapatia ujuzi, kuimarisha uwezo wao wa kujiajiri na kuendelea kuwa na maendeleo endelevu katika shughuli za kiuchumi.

Katika hafla hiyo Waziri Sangu amekabidhi mashine ya ufundi seremala, mashine za saluni, jokofu (fridge) pamoja na bajaji kwa wanufaika hao.

Akizungumza kuhusu programu hiyo Mkurugenzi wa COMHESWA Bwa.Furaha Dimitrios alisema shirika lake linashirikiana na serikali kutafuta fursa za ajira nje ya nchi ambapo vijana wanaunganishwa na waajiri wa nje kwa kupatiwa ujuzi na pindi wanaporejea nchini baada ya kumaliza mikataba yao hupatiwa vitendea kazi ili waendeleze ujuzi walioupata nje ya nchi.

Pamoja na kukabidhi vitendea kazi hivyo, COMHESWA itagharimia ulipaji wa pango( kodi) eneo kwa kila kijana kwa kipindi cha miezi sita ikiwa ni sehemu ya utekelezaji mikataba.