Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Prime Minister's Office

Labour, Youth, Employment and Persons with Disability

News

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA BODI MPYA YA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII (NSSF)



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amezindua Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF), jijini Dodoma Jumamosi Oktoba 27, 2018.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Jenista Mhagama amesema, Waziri Mhagama amesema kuwa mifumo ya kielektroniki itasaidia kuimarisha makusanyo na matumizi ya fedha ndani ya shirika hilo.


“Wekeni mkakati ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato ikiwemo kuhakikisha kuwa mnaimarisha mifumo ya kielektroniki kuongeza mapato na kuongeza tija kwa kuwa mifumo hii itasaidia katika kudhibiti mapato ya mfuko,” Alisisitiza Mhe. Mhagama

Akifafanua mhe. Mhagama amesema kuwa sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi ambapo mpaka sasa sekta hiyo imewekeza jumla ya trilioni 11.79 katika miradi mbalimbali.

Akizungumzia miradi inayotekelezwa amesema kuwa ni pamoja na miundombinu, vifaa tiba na elimu ambayo inaleta tija katika kuchochea maendeleo ya Taifa na ustawi wa wananchi.

Aliongeza kuwa, suala la ujenzi wa uchumi wa viwanda mfuko una jukumu la kuhakikisha kuwa miradi yote inayotekelezwa inalenga katika kuimarisha hali ya uchumi kupitia katika ujenzi wa viwanda.

“Bodi hii imesheheni wataalam wanaoaminika, tunaamini wataenda kuondoa changamaoto mbalimbali zinazokabili shirika hilo,” Alisisitiza Mhe. Mhagama.


Akifafanua amesema kuwa Bodi hiyo inalo jukumu la kufanya usimamizi bora wa mapato ambao utaendana na utengenezaji wa mifumo bora ya kielekitroniki ili kuimarisha usimamizi wa fedha za mfuko huo.

Mhe. Waziri pia ameitaka bodi hiyo kuhakikisha kila mara inafanya tathmini na kujiridhisha kama kuna miradi itakayoanzishwa au iliyopo inasuasua bodi inapaswa kuinasua kwa kuchukua hatua na kufanya maamuzi sahihi kwa wakati ili kujenga imani kwa wanachama.” Alisema.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi, Balozi Ali Iddi Siwa alimuhakikishia Mhe. Waziri kuwa bodi yake itafanya kazi kwa weledi na umakini mkubwa ili kufikia matarajio ya serikali ya kutoa usimamizi ulio bora.

Bodi hiyo inayoongozwa na Balozi Ali Iddi Siwa pamoja na Wajumbe wa bodi wakiwemo Bi. Jane Nyimbo Taylor, Bw. Pelesi Jonathan, Bw.David Magese, Bw.Fred Hans Kipamila, Dkt.Elirehema J. Doriye na Bw. Ahmed A Msaki.


Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Dkt. Irene Isaka na viongozi wengine.